Shughuli ya kuwasajili Wapiga Kura Kumalizika leo

Shughuli ya kitaifa ya kuwasajili wapiga kura itafikia tamati leo jioni. Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC inawahimiza wananchi kujitokeza kusajiliwa kuwa wapiga kura kabla ya muda huo kukamilika. Tume hiyo imeeleza kuridhika na idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wamejisajili kufikia sasa. Hata hivyo tume hiyo imefutilia mbali uwezekano wa kuongezwa kwa muda wa usajili ikisema inahitaji muda huo kukamilisha utaratibu wa uchaguzi. Wakati huo huo tume hiyo inawashauri Wakenya waliojiandikisha wakitumia pasipoti ambazo muda wake wa kutumika umekamilika kutoa nambari za pasipoti zao mpya kwa tume hiyo. Wale ambao wangependa kubadilisha vituo vya upigaji kura wanaweza kufanya hivyo kwenye makao makuu ya maeneo bunge wanayotaka kuhamia wala sio kwenye vituo vya usajili.