Shirikisho la waajiri humu nchini latoa wito kwa waajiri kushauriana kuhusu mishahara na wafanyikazi

Shirikisho la waajiri hapa nchini limetoa wito kwa waajiri na wafanyikazi kushauriana kuhusu mishahara ili kupunguza A�idadi inayoongezeka yaA� A�watu wanaotafuta ajira katika nchi za nje. Mkurugenzi mkuu wa shirikisho hilo A�Jackline Mugo A�amesema kuwa mashauriano ya mara kwa mara kati ya pande hizo mbili kuhusu mishahara pia yatapunguza mizozo inayohusiana na ajira kama iliyoshuhudiwa katika miezi michache iliyopita na hivyo kuchangia kuimarika kwa uchumi wa nchi . Shirikisho hilo limetoa tahadhari kuhusu idadi inayoongezeka ya wafanyikazi wenye ujuzi wanaoendelea kutafuta ajira katika mataifa ya nje ili kujipatia mishahara bora. Alisema hayo wakati wa mkutano wa kila mwaka wa shirikisho hilo ulioandaliwa mjini A�Nakuru na kuhudhuriwa na waakilishi kutoka mashirika mbali mbali na wafanyabiashara katika eneo la Rift Valley.Alisema mizozo ya mishahara kati ya waajiri na wafanyikazi imesababisha migomo ambayo imelemaza ukuaji wa huduma muhimu kama vile afya na elimu . A�