Shirika la ujasusi Marekani limesema halina ushahidi dhidi ya Trump

Shirika la ujasusi nchini marekani imesema kuwa halina nakala zozote za kanda zilizorekodiwa kwenye ikulu ya White House Donald Trump akiwa rais. Shirika hilo lilisema haya A�kwani Trump hajabainisha wazi iwapo kulikuwa na kanda zozote zilizonakili mawasiliano yake ya kibinafsi na aliyekuwa miurugenzi wa shirika la FBI James Comey. Trump aliibua wasiwasi kuhusiana na uwekezano wa kuwepo kwa kanda hizo mwezi uliopita baada ya kumfuta kazi Comey. Aliwaambia wanahabari juma lililopita kwamba atazngumza kuhusu uwezekano huo hivi karibuni. Shirika hilo lilisema hayo kufuatia ombi la uhuru wa kupata habari lililotolewa na jarida moja nchini marekani. Jarida hilo lilisema kuwa huenda kuna uwezekano kwamba asasi nyingine ilinakili mawasiliano hayo.