Huduma mpya ya treni ya kisasa yaanzishwa

Shirika la reli hapa nchini litaanzisha huduma ya pili ya treni kwenye reli ya kisasa kati ya jiji la Nairobi na Mombasa kuanzia leo. Huduma hiyo ya moja kwa moja itaanzishwa katika vituo vya miji ya Nairobi na Mombasa saa tisa unusu mchana.A� Shirika hilo limekuwa likitoa huduma ya moja kwa moja ya treni saa za asubuhi pekee.A� Hatua ya kuzindua huduma ya kwanza ya treni almaarufu Madaraka Express mnamo Julai mosi ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, ilinuiwa kupunguza gharama na kurahisisha usafiri kati ya majiji hayo mawili. Shirika la reli hapa nchini, limeshuhudia ongezeko la abiria ambao sasa hupendelea kusafiri kwa treni. Wateja watahitajika kulipia nauli zao angalau siku tatu kabla ya safari, ili kujikatia tikiti. Treni hiyo itasimama katika vituo-7 vikiwemo Mariakani, Miasenyi, Voi, Mtito Andei, Kibwezi, Emali na Athi River. Shirika hilo limeanza kutoa tikiti kupitia ujumbe mfupi ili kuepusha wafanyibiashara haramu ambao awali walinunua tikiti na kisha kuziuza tena kwa bei ya juu ili kujipatia faida.