Shirika la msalaba mwekundu laonya kwamba hali ya ukame inazidi kuzorota

Shirika la msalaba mwekundu nchini limeonya kwamba hali ya ukame iliyoko sasa inazidi kuwa mbaya zaidi huku mvua za masika zikizidi kuchelewa. Afisa mmoja wa shirika hilo Ahmed Idris amesema hali ya ukame iliyoko sasa humu nchini tayari imefikia kiwango cha kusikitisha na utabiri wa hali ya hewa kuhusiana na mvua za masika za kipindi cha mwezi Marchi hadi Mei A�unaonyesha kwamba hakutakuwa na mvua za kutosha, ijapo baadhi ya maeneo ya humu nchini yameanza kupokea mvua hizo. Akiongea kwenye afisi za shirika la msalaba mwekundu, Idris aliongeza kwamba kwa sasa wanachunguza upya ombi lao kuhusu idadi ya watu wanaofaa kupewa usaidizi chini ya mpango wa kupambana na athari za ukame katika maeneo mbali mbali ya humu nchini. Joyce Kimutai wa idara ya utabiri wa hali ya hewa , anasema hali ya ukame iliyoko sasa huenda ikawa mbaya zaidi kwa kulinganisha na kipindi cha mwaka 2010/2011 A�ambapo watu milioni-3.7 waliathiriwa. Katika ripoti yake kwa kikao cha kutathmini hali ya ukame nchini Kenya, mwaka 2016/2017 kilichoandaliwa katika hoteli moja Jijini Nairobi idara ya utabiri wa hali ya hewa ilisema maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na Mandera, Marsabit, Garissa, Isiolo, Kwale, Turkana, Pokot Magharibi, Samburu, Tana River, Kilifi, Wajir na Lamu ambako hali hiyo imefikia kiwango cha kusikitisha, na kwamba A�baadhi ya maeneo hayo huenda yakahitaji chakula cha dharura katika muda wa wiki chache zijazo.