Shirika la msalaba mwekundu latoa wito wa misaada zaidi kwa waathiriwa wa kimbunga

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limetoa wito wa kutolewa kwa misaada kwa maelfu ya watu walioachwa bila makazi kutokana na kimbunga cha cyclone nchini Madagascar. A�Shirika hilo limesema kuwa watu kadhaa walifariki, wengine A�200 wakajeruhiwa huku wengine zaidi ya elfu 80 wakiachwa bila makazi kutokana na kimbunga hicho cha juma lililopita. Shirika hilo linaongeza kuwa kimbunga hicho kiliharibu mali, kusababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko hali ambayo inafanya kuwa vigumu kufikia maeneo yaliyoathirika. A�Shirika hilo limesema kuwa watu wanahitaji chakula, makazi, matibabu, maji safi na bidhaa nyingine za kimsingi.