Shirika La KWS Latoa Tahadhari Kuhusu Simba Waliotoweka

Shirika la kuhifadhi wanyama hapa nchini limetoa tahadhari kuhusu kutoweka kwa simba wawili wa kike kutoka mbuga ya kitaifa ya Nairobi. Simba hao yaaminika walitorokea katika eneo la Langa��ata ambalo linapakana na mbuga hiyo. Afisa wa mawasiliano wa shirika hilo, Paul Udoto amesema wanategemea wananchi kutoa habari kuhusu waliko simba hao. Udoto amesema simba hao walionekana karibu na hopitali ya Lang’ata mapema leo na kuonya wananchi dhidi ya kujaribu kuwashambulia kwani ni hatari.