Shirika la huduma za feri kufahamu iwapo litazindua feri mpya

Shirika la huduma za feri KFS leo tarehe mosi mwezi Augosti A�litajua iwapo litaweza kuzindua moja wapo wa feri zake mbili mpya iliyonunuliwa kwa kitita cha shilingi bilioni mbili kutoka Uturuki. Kupitia wakili wake, shirika hilo linataka mahakama kubatilisha agizo la kusitisha uzinduzi wa feri hiyo ya A�MV Jambo iliyowasili siku ya alhamisi hadi itakapofanyiwa ukaguzi. Uamuzi wa Jaji wa mahakama kuu Erick Ogola hivi leo utabainisha iwapo shida zilizoko sasa katika usafiri kupitia kivuko cha Likoni zitapunguzwa. Feri hizo mbili zina uwezo wa kubeba abiria 1,391 kila moja. Maslahi ya watu wanaoishi na ulemavu, wakongwe na pia Kina mama wajawazito na wagonjwa pia yametiliwa maanani. Huduma nyingine ambazo hazipatikani kwa sasa katika A�feri hiyo ni pamoja na vyoo. Ili kuboresha usalama feri hiyo itakuwa ikibeba pia mashua mbili za uokoaji na maswala ya dharura.