Shindano la viatu vinavyotoa uvundo mkali zaidi

Vijana saba hivi majuzi walishiriki kwenye shindano kuhusu ni nani aliye na viatu vinavyotoa uvundo zaidi mjini New York, Marekani. Connor Slocombe mwenye umri wa miaka-12 aliibuka mshindi katika jaribio lake la tatu na kunyakua taji hilo. George Aldrich, mtaalamu wa masuala ya kemikali alisema Slocombe alifaulu kuwa na uvundo zaidi kwenye viatu vyake. Shindano la viatu vinavyotoa uvundo mkali zaidi lilianzishwa mwaka 1974 na mmiliki wa duka la kuuza viatu katika eneo la Vermont kama njia moja ya kupendekeza viatu vipya. Kampuni ya Odor-Eaters ilianza kudhamini shindano hilo mwaka 1988.