Shehena ya kwanza ya karatasi za uchaguzi wa urais zawasili hapa nchini

Shehena ya kwanza ya karatasi za uchaguzi wa urais iliwasilini A´┐Żnchini jana jioni. Karatasi za uchaguzi kwa kaunti 30 zilipokewa na maafisa wa tume ya IEBC katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Karatasi hizo za uchaguzi zilizochapishwa na kampuni ya uchapishaji ya Dubai ya Al-Ghurair ziko katika vijitabu 416,360 na kila kijitabu kina kurasa 50. Karatasi za uchaguzi wa urais ni 20,818,00 dhidi ya wapiga kura 19,646,673 waliosajiliwa ambapo zinajumuisha asilimia moja ya karatasi za ziada za kura ambazo huenda zikaharibika.