Seth Panyako adumisha kwamba mgomo wa wauguzi utaendelea

Katibu mkuu wa chama cha wauguzi cha KNUN, Seth Panyako, amedumisha kwamba mgomo wa wauguzi utaendelea hadi maafikiano ya pamoja yatakaposajiliwa mahakamani na kutekelezwa. Akiongea jana na wanahabari jijini Nairobi, katibu huyo mkuu alishutumu serikali za kaunti na ile ya taifa kwa kutokuwa na nia ya kutatua mzozo huo.A� Aidha Panyako aliishutumu tume ya kushughulikia mishahara hapa nchini-SRC kwa kutowajibika katika ripoti yake ya utathmini wa kazi wa hivi pundeA� iliyotolewa na tume hiyo inayoongozwa na Sarah Serem. Wakati uo huo,A� Panyako amewapa wauguzi katika kaunti ya Nandi saa 24 kurejea mgomoni, akisema Gavana Stephen Sang, aliwabagua katika makubaliano yao ya hivi punde. Hata hivyo, Panyako alisema chama hicho kiko tayari kwa mashauriano ya kutatua mzozo huo ambao umedumu kwa takriban miezi minne sasa. Panyako kwa sasa ametoa wito wa kufungwa kwa taasisi zote za mafunzo ya matibabu hapa nchini, kwa sababu ya mgomo huo.