Serikali yatuma msaada wa chakula kwa waathiriwa wa mafuriko Kaunti ya Taveta

Serikali ya kitaifa imesambaza magunia elfu 1 ya kilo 50 ya mahindi , magunia 250 na katoni 50 ya mafuta ya kupikia kwa waathiriwa wa mfuriko katika kaunti ndogo ya Taveta . Kulingana na naibu kamishna wa kauntiA� Henry Wafula, msaada huo unanuia kuwasaidia wakazi wa eneo hilo ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko wiki iliyopita. Maeneo yalioathirika zaidi ni pamoja naA� Kimorigo, Challa, Njoro, Bura Ndogo, Mata, Jipe na Riata. Wakati huo huo wakazi wanaoishi katika maeneo yanayokabiliwa na athari ya kukumbwa na mafuriko katika kaunti ya A�Baringo wametakiwa kuhamia maeneo salama huku mvua inayoendelea kunyesha ikitarajiwa kuendelea . Baadhi ya maeneo ya Ilchamus, Mochongoi, Emining na maeneo ya chini yaA� Baringo Kusini na Kaskazini huenda yakaathirika kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi . Naibu gavana wa kaunti ya Baringo Mathew Tuitoek hata hivyo amewahakikishia wakazi kuwa hatua madhubuti zimewekwa ili kushughulikia mikasa yoyoye itakayotokea. Kwengineko takriban watu 300 wamepoteza makao katika lokesheni ya Usonga katika kaunti ya Siaya kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha katika siku mbili zilizopita. Kulingana na naibu wa chifu wa lokesheni ndogo yaA� Nyadorera ‘B’ Felix Odongo, mkasa huo ulikumba eneo la baada yam toA� Hwiro Mahur kuvunja kingo zake na kusomba nyumba 46 siku ya Jumatano usiku. Odongo alisema kuwa vijiji vya Mahur, Uhembo na Nyangera ndivyo vilivyoathirika zaidi na kwamba watuA� 298 wameagizwa kutafuta makazi ya muda kuepukana na hasara ya maisha ya mali.A� Chifu huyo alitoa wito kwa taasisi za serikali pamoja na mashirika ya kibinadamu kuwasidia wale walioathirika kwa makazi, chakula na nguo. .