Serikali yatenga shilingi bilioni 2.1 kwa miradi ya maji

Serikali ya kitaifa itafadhili miradi ya maji kwa kima cha shilingi bilioni A�2.1 katika kaunti saba zilizoko katika maeneo kame ya Kaskazini mwa Kenya. Miradi hiyo inayojumuisha uchimbaji vidimbwi, mabwawa na visima na itatekelezwa katika awamu kadhaa na kukamilika katika kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu. Miradi hiyo inatekelezwa katika kaunti za Garissa, Isiolo, Marsabit, Wajir na Samburu. Akitaarifu wanahabari katika eneo la Abakaile, kaunti ndogo ya Dadaab ambako alikagua kidimbwi cha maji kilichochimbwa kwa gharama ya shilingi milioni-36,A� katibu katika wizara ya maji Prof Fred Segor alisema miradi hiyo inanuiwa kupunguza mwendo ambao wakazi hutembea kutafuta maji. Kidimbwi cha maji cha Abakaile ambacho kimekamilika kwa asilimia- 80 kinatarajiwa kunufaisha familia 6,000 na mifugo 140,000 .