Serikali yatekeleza marekebisho kwenye sekta ya kahawa

Serikali inatekeleza marekebisho kwenye sekta ya Kahawa ambayo yatawezesha wakulima wenye mashamba madogo kuongeza uzalishaji. Mikakati hiyo mpya inalenga kushughulikia gharama ya juu ya uzalishaji na changamoto katika ununuzi wa mbegu  ambazo huathiri uzalishaji.  Mnamo mwaka uliopita Rais Uhuru Kenyatta aliteuwa  jopo kazi la wanachama 19 la kubuni na kutekeleza kanuni mpya ambazo zitaifufua sekta ya Kahawa.  Kamati hiyo ya tekelezi  ya  kitaifa kuhusu sekta ndogo ya Kahawa inawataka wadau kuunga mkono utekelezaji wa  marekebisho hayo ili kuwanufaisha wakulima na taifa kwa jumla.  Marekebisho hayo yanalenga kupunguza gharama ya uzalishaji kwa kupunguza bei ya  pembejeo na kuwapa wakulima mafunzo