Serikali yataka watumishi wa umma kudhibiti ajali mbaya barabarani

Serikali imewataka watumishi wa umma wanaohusika na udumishaji usalama barabarani kusaidia katika kudhibiti ajali mbaya kwenye barabara za humu nchini. Akiongea hapa Nairobi,msemaji wa serikali Eric Kiraithe alisema hatua itachukuliwa dhidi ya watumishi wa umma ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.Kiraithe alisema ajali za barabarani ambazo zimetokea katika muda wa siku chache zilizopita na kusababisah vifo vya zaidi ya watu 70,zimesababishwa na makosa ya kibinadamu.Msemaji huo wa serikali alitoa wito kwa tume ya kukabiliana na ufisadi nchini kushirikiana na maashirika mengine wa kudumisha sheria ili kuangamiza ufisadi kwenye barabara za humu nchini,jambo ambalo alidai limechangia pakubwa kuongezeka kwa ajali hizo za barabarani.Huku akisema hayo,watu wawili waliripotiwa kufanriki baada ya lori mbili kugongana karibu na sehemu ya Malili kwenye barabara kuu kati ya Nairobi na Mombasa.Kulingana na afisa mkuu wa polisi huko Mukaa Charles Muthui, dereva na turn-boi wa moja wa lori hizo walifariki huku abiria waliokuwa kwenye lori la pili wakipata majeraha mabaya na kupelekwa kwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Machakos.