Serikali yapiga marufuku uagizaji wa mahindi kutoka nchi jirani

Serikali imepiga marufuku uagizaji mahindi kutoka nchi jirani licha ya nakisi ya magunia milioni nane inayokumba nchi hii . Kulingana na katibu katika wizara ya kilimo Richard Lesiyampe serikali itawapa motisha wakulima kupitia bora kuuza mahindi yao kwa halmashauri ya kitaifa na nafaka na mazao NCPB ili kuondoa upungufu ambao umetokana na mavuno duni. Lesiyampe amesema kwa miaka mingi nchi hii imekuwa ikikosa kutimiza mahitaji yake ya mahindi na kulazimika kuagiza mahindi kutoka nchi jirani za Uganda naA� Tanzania Katibu huyo amekariri nia ya serikali kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa mahindi.