Serikali yaondoa ushuru wa uagizaji sukari

Serikali imeondoa ushuru wa uagizaji sukari kutoka kwa mataifa wanachama wa shirika la soko la pamoja la mataifa ya kusini mwa Afrika-COMESA kwenye jaribio la kukabiliana na ongezeko la bei za sukari. Hatua hii inajiri wakati ambapo serikali imeagiza mahindi kutoka Mexico, Ethiopia na Afrika kusini ili kuthibiti bei za unga wa mahindi hapa nchini.