Serikali Yaimarisha Usalama Nchini

Serikali imeimarisha usalama kwenye viwanja vyote vya ndege hapa nchini huku ikiwahakikishia wasafiri na wageni kuwa safari za ndege za hapa nchini na kimataifa ni salama. Kwenye taarifa ya pamoja iliyotumwa na waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Nkaisserry na mwenzake wa utalii Najib Balala, serikali imesema maafisa wa usalama wanajibidiisha kuhakikisha usalama umedumishwa kote nchini. Hakikisho hilo limefuatia arafa ya halmashauri ya viwanja vya ndege hapa nchini kuhusu vitisho vinavyokabili viwanja vya ndege kufuatia mashambulizi ya kigaidi. Aidha taarifa hiyo imesema maafisa wa usalama watajikakamua kuhakikisha wananchi na wageni wako salama popote walipo.