Wamalwa aeleza mpango wa kumaliza uhaba wa maji Nairobi

Maafisa wa wizara ya maji na unyunyiziaji mashamba maji wakiongozwa na waziri Eugene Wamalwa,A� jana walimuarifu Rais Uhuru Kenyatta kuhusu miradi inayotekelezwa na serikali katika juhudi za kumaliza upungufu A�wa maji wa lita milioni-250 jijini Nairobi. Jiji hilo hupokea lita millioni 520 za maji kila siku kwa kulinganisha na mahitaji yake ya lita millioni 750. Mradi utakaokamilika hivi karibuni wa a�?Northern Water Tunnela�? kutoka Murang’a, unatarajiwa kuongeza kiwango cha maji jijini Nairobi kwa lita A�millioni 140. A�Kiwango kingine cha lita milioni 100 za maji au zaidi kitasambazwa katika Jiji hilo kupitia ujenzi, na kukamilika kwa miradi ya mabwawa ya Karimeni 2 na Ruiru 2. Aidha, Wamalwa alimfahamisha Rais kuhusu miradi sambamba ya kuhakikisha miji A�ya Mombasa, Kisumu na Nakuru inajitosheleza kwa maji. Kulingana na waziri huyo, mji wa Kisumu utakuwa wa kwanza kujitosheleza kwa maji baada ya kukamilishwa kwa mradi wa maji wa Kisumu. Wakati huo huo, huduma za maji mjini Mombasa zitaboreshwa na kukamilishwa kwa bwawa la maji la Mwache na pia bomba la maji la Mzima Springs 2. Mji wa Nakuru utajitosheleza kwa maji A�baada ya kukamilika kwa bwawa la maji la Itare. Mpango wa kuboresha huduma za maji katika miji hiyo muhimu zaidi nchini, ni sehemu ya mpango wa serikali wa kuongeza mara tatu uwezo wa kuhifadhi maji katika taifa hili, na pia kuongeza idadi ya wakenya walio na huduma bora za maji kutoka asilimia 60 kwa sasa hadi asilimia 80 itimiapo mwaka 2020. Serikali inatekeleza miradi mikubwa 60 ya mabwawa ya maji kote nchini, mbali na jitihada zake za kuhakikisha kwamba Jiji la Nairobi na pia miji mingine muhimu hapa nchini inajitosheleza kwa maji kufikia mwkaa 2020.