Serikali Yahamasisha Ukuzaji Wa Talanta Kwa Ujenzi wa Kituo Kipya Cha Utamaduni

Serikali imezindua kituo kipya cha utamaduni na baraza la masuala ya utamaduni kusaidia kukuza talanta hapa nchini. Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi katika hoteli ya Mombasa, waziri wa michezo n utamaduni Hassan Wario alisema fedha zimetengwa kufadhili baraza hilo. Alisem baraza hilo limebuniwa kuhkikisha wasanii na wachezaji filamu wananufaika na biashara hiyo. Alisema wakati uliopita wasanii wengi hawajanufaika na talent zao hali ambayo imewasabisha wao kuwa maskini. Aliongeza kusema kuwa baraza hilo pia linatarajia kusimamia uzinduzi wa kituo cha kimataifa cha usanii na utamaduni kuambatana na ruwaza ya mwaka 2030. Bodi ya baraza hilo inajumuisha Nicholas Ole Mpoipei, ambaye ni mwalimu wa muziki, Wachira Waruru wa baraza la wanahabri n Edward Muthusi atakuwa meneja wa matangazo. Wengine ni Liucas Manyasi, Millicent Ogutu, Bi. Alison, Saima Ondimu na David Keter. Wario pia aliahidi kujitolewa lwa serikali kuimarisha usanii na utamaduni hapa nchini.