Serikali Yafanyia Mabadiliko Muhula Wa Pili Na Wa tatu Katika Shuze Za Msingi Na Sekondari

Serikali imeongeza muda wa muhula wa pili kwa shule zote za msingi na sekondari kwa wiki moja na kupunguza muda wa muhula wa tatu. Muhula wa tatu kwa shule zote za msingi na sekondari utaanza Agosti 29 na kumalizika Oktoba 28 kwa darasa la kwanza hadi la saba na kidato cha kwanza hadi cha tatu ili kuwaruhusu wanafunzi wa kidato cha nne kufanya mtihani kuanzia Novemba 7 mwaka huu bila kutatizwa. Dr. Matianga��i alitangaza hayo baada ya kufanya mkutano wa faragha na maafisa wa wizara ya Elimu na wenzao wa Baraza la kitaifa la mitihani, Tume ya kuwaajiri walimu (TSC), Taasisi ya maendeleo ya mtaaka nchini (KICD),na vile vile maafisa wa chama cha walimu wakuu wa shule za sekondari (KESSHA).

Serikali pia imepiga marufuku shughuli zote za kijamii vikiwemo vikao vya maombi kwa wanafunzi katika muhula wa tatu vinavyowapa wazazi na watu wengine kutembelea shule wakati wa muhula wa tatu.A� Hata hivyo matayarisho ya maombi na ibada yanayohusu makasisi wa shule na walimu hayataathiriwa.

Aidha waziri alisema walimu wakuu wa shule kwa mara ya kwanza watawajibika kwa shule zao kama vituo vya mitihani zitakapochaguliwa na Baraza la kitaifa la mitihani nchini. Mtihani wa darasa la nane KCPE utaanza Novemba 1 na kumalizika Novemba 3. Alisema hatua alizochukua kulinda hadhi na uaminifu wa mitihani zilifikiwa kupitia mpango wa ushauri wa wadau wa elimu