Serikali yaagizwa kuanzisha miradi ya kutatua shida za kudhulumiwa kwa mtoto wa kiume

Kumekuwa na ongezeko la dhuluma dhidi ya mtoto wa kiume katika siku za hivi majuzi, jambo ambalo linahatarisha maisha yao. Mwenyekiti wa chama cha Maendeleo ya Wanaume Ndiritu Njoka ameitaka serikali kuanzisha miradi ya kutatua tatizo hilo. Njoka alisema haya katika kijiji cha Mataara eneo la Gatundu Kaskazini wakati wa sherehe ya kumkaribisha nyumbani mvulana wa miaka mitano ambaye alikuwa amelazwa hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye sehemu za siri na mwalimu wake kwa madai ya kupiga kelele darasani mwezi uliopita. Njoka alimpongeza aliyekuwa mbunge wa sehemu hiyo Kungu Waibara A�kwa kugharamia matibabu ya mvulana huyo.