Serikali ya Uganda ina mipango ya kutoza kodi watumiaji mitandao ya kijamii

Serikali ya Uganda ina mipango ya kutoza kodi watumiaji wa mitandao ya kijamii kuanzia mwezi Julai mwaka huu ili kukusanya mapato.Haya yametangazwa na waziri wa fedha wa nchi hiyo Matia Kasaija.Hata hivyoA� pendekezo hilo limeshutumiwa vikali na mwanaharakati wa haki za binadamu Rosebelle Kagumire,ambaye ametaja hatua hiyo kuwa ukiukaji waA� haki ya kujieleza.

Mapema mwezi huu,Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa mamlakani kwa zaidi ya miaka 30 alinukuliwa na gazeti moja akimtaka waziri wa fedha kuwatoza kodi wale wanaotumia mitandao ya kijamii kueneza umbeya.Kodi hiyo iliopendekezwa itatozwa kila rununu iliyo na mitandao ya kijamii ya WhatsApp,Facebook na Twitter,kwa mujibu wa shirika la habari la REUTERS.Hata hivyo kiwango cha kodi yenyewe hakikutajwa