Serikali ya Uchina kushirikiana na kenya katika kuimarisha ustawi wa viwanda

Serikali ya Uchina imeahidi kuunga mkono juhudi za Kenya za kujenga maeneo ya kibiashara karibu na reli ya kisasa kama sehemu ya kuimarisha ustawi wa viwanda hapa nchini. Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa viwanda karibu na vituo vya reli hiyo mijini Mombasa na Nairobi na karibu na uwanja wa ndege. Naibu waziri wa mashauri ya kigeni wa uchina anayezuru hapa nchini Zhang Ming alipuuzilia mbali wasiwasi kuhusu deni la kitaifa la Kenya akisema reli hiyo ya kisasa itafanikisha ustawi wa viwanda hapa nchini na kupiga jeki uchumi wa taifa. Zhang alisema ikiwa deni hilo litatumiwa ipasavyo, litakuwa na manufaa katika ustawi wa taifa na utoaji ajira hapa nchini.