Serikali ya Tanzania yataka Umoja wa Mtaifa kuanzisha uchunguzi dhidi ya mauaji ya wanajeshi wake

Serikali ya Tanzania imeutaka Umoja wa Mtaifa kuanzisha uchunguzi dhidi ya mauaji ya wanajeshi wake 14 wiki iliyopita wakidumisha amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. Katika mazishi yaliyogubikwa na huzuni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alisema familia pamoja na serikali wataka kufahamu hasa kipi kilifanyika. Majaliwa alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuendehs uchunguzi wa kina na wazi kufuatia umwakigaji huo wa damu ya wanajeshi wa Tanzania kwa lengo la kutimiza haki. Alitumai kwamba hayo yatatimizwa katika muda mfupi. Waziri huyo Mkuu alielezea shambulizi hilo kuwa baya zaidi katika muda wa robo karne dhidi ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanodumisha amani. Umoja wa Mataifa unaamini kundi la waasi la Alliance for Democratic Forces la Uganda lilihusika ingawa hilo halijathibitishwa.