Serikali ya Mugabe huenda imepinduliwa na jeshi

Hatua ya jeshi la Zimbabwe ya kutwaa mamlaka na kumzuilia rais Robert Mugabe inaonekana kuwa kama ya mapinduzi ya serikali kwa mujibu wa muungano wa Afrika. Mwenyekiti wa muungano wa Afrika Alpha Conde anasema muungano wa Afrika unataka nchi hiyo kurejelea utawala wa kikatiba mara moja. Hata hivyo jeshi limekanusha kutekeleza mapinduzi ya kijeshi, likisema Mugabe yu salama na sasa linakabiliana na wahalifu wanaomzingira. Hatua ya jeshi inafuatia kinyanga��anyiro cha uongozi kuhusu ni nani atakayemrithi Mugabe. Makamu wake wa rais Emmerson MnangagwaA� alifutwa kazi wiki iliyopita na hivyo kutoa fursa kwa mkewe Mugabe, Grace kuwa ambaye anaweza kumrithi hukuA� maafisa wakuu wa kijeshi wakihisi kutengwa. Mugabe mwenye umri wa miaka 93, amethibiti ulingo wa siasa katika taifa hilo linaloghubikwa na umaskini tangu lililpopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1980.