Serikali ya Garissa kuzindua huduma za afya ya uzazi

Serikali ya kaunti ya Garissa itazindua huduma za afya ya uzazi kwa lengo la kuimarisha hali ya afya na lishe bora kwa wanawake na watoto katika kaunti hiyo. Akiongea wakati wa uzinduzi wa mwezi wa Malezi Bora mjini Garissa, ambao kauli mbiu yake ni a�?Afya ya Jamii, Ustawi wa Nchi, katika kaunti ya Garissaa�? afisa mkuu wa afya, Ahmednadhir Omar, alisema kwamba idara yake itazingatia mikakati ambayo itajumuisha chanjo kwa watoto, huduma za upangaji uzazi, utoaji dawa za vatamini A, kuwapa watoto dawa za minyoo na huduma za afya ya uzazi kwa kina mama. Afisa mkuu huyo wa afya aliyahimiza makundi ya kijamii, mashirika ya umoja wa mataifa na washirika wengine kuunga mkono kampeni hiyo ya uhamasisho ambayo inanuiwa kuwasaidia wanawake wajaa wazito kwenda katika vituo vya afya ili kupokea huduma za kitaalam za afya ya uzazi. Alisema mbali na hatua hii kupunguza hatari za matatizo ya kujifungua pia itawapa wanawake fursa ya kupokea elimu ifaayo kuhusu unyonyeshaji watoto na lishe bora.