Serikali Ya Congo Yashutumu Mashambulizi Ya Majengo Yake Mjini Brazzaville

Serikali ya Congo imeshutumu mashambulizi yaliotekelezwa dhidi ya majengo ya serikali katika mji mkuu ,Brazaville,ambayo inadai yalitekelezwa na kundi moja la kigaidi.Wanajeshi wa taifa hilo walipelekwa katika sehemu tofauti za mji huo A�siku ya jumatatu kurejesha utulivu baada ya milio ya risasi na bunduki za rashasha kusikika kwenye barabara kuu.Iliarifiwa kuwa kituo kimoja cha polisi na jengo moja la polisiA� katika wilaya ya Makelekele vilishambuliwa.Walinda usalama walipelekwa kulinda maeneo muhimu ya mji huo.Ghasia hizo zinajiri wiki kadhaa baada ya rais Dennis Sassou Ngwesso kushinda awamu ya tatu ya utawala,kwenye uchaguzi ambao upinzani ulidai kuwa A�ulikumbwa naA� udanganyifu.Kundi hilo la wapiganaji lilikuwa na uhusiano wa karibu na aliyekuwa waziri mkuuA� Bernard Kolelas,babake Guy-Brice Parfait Kolelas ambaye aliwania urais mnamo mwezi wa Machi na kupata aslimia 15 ya kura.Rais Sassou Ngwesso ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka 30,alishinda uchaguzi huo kwa aslimia 60 ya kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *