Serikali wahimizwa kushirikiana na wanahabari kukuza michezo Barani Afrika

Kuna haja ya serikali kushirikiana na wanahabari kwa nia ya kuendeleza na kukuza michezo katika Bara Afrika. Katibu katika wizara ya michezo Ambassador Peter Kaberia aliwashukuru wanahabari wa michezo humu nchini kwa kujikaza kuwasilisha habari zinaoisuta wizara ya michezo. Kaberia alisema hayo baada ya kufungua rasmi kongamano la chama cha kimataifa cha wanahabari wa michezo AIPS barani Afrika. Kwa siku mbili wanahabari wa michezo kutoka mataifa 26 wanakongamana katika jiji la Nairobi ili kujadiliana kuhusu maswala yanayowakumba wanahabari wa michezo na jinsi ya kuboresha taaluma ya uanahabari wa michezo. Huku akifungua rasmi kongamano hilo, Katibu katika wizara ya michezo Ambassador Peter Kaberia aliwataka wanahabari kuwajibika katika ripoti wanazowasilisha kwa umma kila kuchao. Ni mara ya kwanza kwa kongamano hilo kundaliwa humu nchini na eneo la Afrika Mashariki.