Serikali kuwajengea nyumba za kisasa maafisa wa polisi ambao nyumba zao ziliteketea kituo cha Central

Serikali itawajengea nyumba za kisasa maafisa wa polisi ambao nyumba zao ziliteketea juma lililopita katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi.A�Akiongea alipozuru kituo hicho, waziri wa usalama wa taifa Fred Matianga��i amesema ujenzi huo utaenda sambamba na mradi mkuu wa serikali wa kuwajengea maafisa wa polisi zaidi ya nyumba elfu ishirini kote nchini.

Waziri alisema serikali tayari imekamilisha mipango ya kujenga nyumba za kisasa kwa zaidi ya maafisa 50 wa polisi wanaohudumu katika kituo cha polisi cha Central jijini Nairobi. Akiongea baada ya kuzuru mahala palipozuka moto huo siku ya Ijumaa, Matianga��i, alikariri kujitolea kwa serikali kuhakikisha maafisa wote wa polisi wana nyumba nzuri hapa nchini.A�Hata hivyo kwa sasa serikali itawatafutia makazi mbadala maafisa wa polisi walioathiriwa na moto huo.

Fred Matianga��i