Serikali Kupitisha Mswada Wa Kukabilana Na Dawa Za Kusisimua Misuli

Rais Uhuru Kenyatta amewahakikishia Wakenya kwamba mswada wa mwaka huu wa kukabiliana na dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha utapitishwa kwa wakati kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na shirika la kimataifa ya kukabiliana matumizi ya dawa hizo -WADA. Rais alisema serikali imetoa kipaumbele kwa mswada huo, akisema yeye binafsi anaufuatilia mswada huo pamoja na uongozi wa bunge la taifa. Rais Kenyatta alisema kufikia mwisho wa juma lijalo, mswada huo utakuwa umepitishwa na bunge na atakuwa ameutia saini kuwa sheria ili kusiwe na sababu yoyote ya kuwazuia wanamichezo wa humu nchni kushiriki kwenye michezo wa Olimpiki mjini Rio de Janeiro, Brazil, mwezi Agosti.Kiongozi wa nchi alisema hayo alipokuwa mwenyeji wa timu za mbio za marathoni za Paris na zile za nusu marathoni duniani kwa hafla ya kiamsha kinywa katika ikulu ya Nairobi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *