Serikali Kukamilisha Ujenzi Wa Kiwanda Cha Kidijitali Nchini

Serikali kwa ushirikiano na washirika wa habari na mawasiliano inakamilisha mipango ya ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha vifaa vya Elimu kwa njia ya digitali A�hapa nchini katika juhudi za kufanikisha mpango huo na kutoa ajira kwa wakenya.Katibu wa ustawishaji wa vyama vya ushirika A�Ismail Noor amesema serikali inadhamiria kujenga kiwanda hicho cha mabilioni ya pesa ili kufanikisha mpango wa elimu kwa njia ya kidijitali na vile vile kuwezesha usambazaji wa vifaa vya kutosha vya elimu ya kidijitali kote nchini.Noor alisema haya katika shule ya msingi ya Kapkewa ilyoko kaunty ndogo ya Kuresoi huko Nakuru alikozindua maabara ya elimu ya kidijitali A�itakayowawezesha wanafunzi mia tatu kunufaika na mpango huo wa elimu mhula huu.Katibu huyo alisema vyuo viku vya Moi na Kenyatta vinatoa utaalam wa kiufundi kwa mpango huo wa elimu kwa njia ya dijitali katika shule za msingi na za secondary.