Serikali Kujenga Vituo Vya Ukarabati Mjini Mombasa

uk
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kwamba zaidi ya shillingi millioni mia tano kwenye kesi ya ufisadi ya Jersey zitatumiwa kujenga vituo vya kuwarekebisha waraibu wa mihadarati na nyumba salama kwa wanawake ili kuwalinda dhidi ya ghasia za kinyumbani.

Rais alisisitiza kwamba serikali yake itaendelea kukabiliana na ufisadi.Rais alisema wale wote wameiba pesa za uma sharti wazirejeshe ili ziwasaidie wakenya masikini.Akiongea katika Ikulu ya Mombasa alipowahutubia zaidi ya vijana elfu nane , wanawake na wazee kutoka kauntI sita za pwani,rais alisema serikali yake imejitolea kushughulikia masuala ya vijana na wanawake.

Kiongozi wa nchi vile vile aliwahimiza wakazi wa pwani kuiunga mkono serikali ya Jubilee ili kuleta maendeleo ya haraka katika eneo hilo.Alitaja miradi kadhaa ambayo serikali yake imetekeleza katia eneo hilo ikiwemo miundo msingi, miradi ya maji na usambazaji stima.