Serikali kuwapa wanafunzi chakula kufuatia ukame nchini

Waziri wa elimu, dakta Fred Matianga��i amesemaA�serikali itaimarisha mpango wa kuwapa wanafunzi chakula kutokana na hali ya ukame inayokumbaA�sehemu nyingi za humu nchini. Matiang’i amesema chakula cha msaada kitasambazwa shuleni kwa ushirikiano na shirika la vijana wa huduma kwa taifa NYS. Dakta Matianga��i pia alimwagiza katibu katika wizara hiyo, dakta Belio Kipsang, kuchapisha orodha ya kaunti zilizoathiriwa zaidi na ukame na kuwataka wasimamizi wa shule kutowatoza wazazi pesa zaidi au kuwafukuza wanafunzi kwa sababu ya karo. Alisema serikali tayari imetenga shilingi milioni 154 ambazo zitagawiwa shule mbali mbali katika kipindi hiki cha kiangazi. AkiongeaA�katika kaunti ya Nyandarua alipotembelea shule kadhaa, waziri Matiang’i aliwataka maafisa wa elimu kufuatiliaA�A�hali hiyo ili kuhakikisha wasimamizi wa shule hawababaiki kutokana na hali ya ukame. Kwa upande wake waziri wa maswala ya vijana na jinsia, Sicily Kariuki alisema chakula cha msaada kinachosambazwa katika maeneo yaliyoathiriwa, kinapelekwa moja kwa moja katika shule zinazohitaji msaada.