Serikali yaanzisha mfumo wa habari inayowalinda watoto

Serikali imeanzishsa mfumo wa usimamizi wa A�habari zinazowalinda A�watoto ili kufuatilia na kushirikisha masuala yanayohusiana na watoto kote A�nchini. Mfumo huo kupitia mtandao A�unaofanyiwa A�majaribio A�katika kaunti 10, utaimarisha uhusiano kati ya A�idara A�ya watoto na mashirika ya msaada. Mkurugenzi wa huduma za watoto katika kaunti ya Kisumu , Humphrey Wandeo, alisema kuwa kupitia mfumo huo , kesi zote na masuala yanayohusiana na watoto yatapatikana mara A�moja A�. Wandeo alisema kuwa maafisa wa watoto katika kaunti ndogo za kaunti zinazofanyiwa majaribio, wanaweka maelezo katika mfumo huo kuhusiana na kesi ambazo wameshughulikia tangu tarehe 1 mwezi Julai mwaka 2016 . Alisema kuwa mfumo huo utaanza kutumika kabla ya kukamilika kwa kipindi cha bajeti cha mwaka huu. Aliongeza kuwa A�mfumo huo unatarajiwa kuimarisha A�ushughulikiaji wa masuala yanayowahusu watoto kwa kuwa itakuwa rahisi kufuatilia kesi hadi tamati .