Serikali Kuanza Kuwachanja Watoto Leo Dhidi Ya Ukambi

Serikali leo itaanza kuwachanja watoto wa umri wa kati ya miezi-9 na miaka-14 ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Ukambi. Kutokana na hayo wazazi wametakiwa kuwasilishwa watoto wao kwa shughuli hiyo itakayoendelea kwa muda wa siku tisa. Wizara ya afya imesema inatarajia kuwachanja watoto wapatao millioni 19 kote nchini. Kaunti 11 zinazolengwa kwenye kampeni hiyo ni Kilifi, Mombasa, Meru, Mandera, Wajir, Garissa, Baringo, West Pokot, Turkana, Samburu na Narok. Wakati huo huo idara ya afya ya umma katika huko Teso Kaskazini imewahakikishia wazazi na wale kuhusu usalama wa chanjo hiyo ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Ukambi. Mbali na chanjo ya kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Ukambi wanawake pia watachanjwa kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa Pepo Punda.Afisa mkuu wa afya ya umma katika kaunti hiyo ndogo James Simiyu alisema kwamba vituo vya kampeni hiyo ya kuwachanja watoto vitakuwa katika shule zote za nasari na msing,vituo vya biashara na kumbi za maombi. A�Alisema kwamba serikali ya Kaunti ndogo ya Teso Kaskazini inalenga kuwachanja watoto alfu-54.