serikali inatafuta suluhu utata kuhusu bei ya mafuta asema Ruto

Naibu wa rais William Ruto ametoa hakikisho kuwa suluhu mwafaka litapatikana ili kutuliza utata unaotokana na ongezeko la bei ya mafuta nchini. Akiongea wakati wa ibada ya maombi katika kanisa katoliki la Good Shepherd katika eneo la North Horr kaunti ya  Marsabit, Naibu Rais alisema kuwa serikali itashirikiana na bunge kutatua utata ulioko.

Wakati huo huo, Naibu wa Rais ametoa wito kwa jamii za wafugaji wa kuhama-hama kukoma kujihusisha na wizi wa mifugo huku akiongeza kuwa inasikitisha kuwa uovu huo unaendelezewa katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa taifa hili wakati ambapo wakenya wengine wanajihusisha na shughuli za kuleta manufaa na kuboresha maisha yao. Alitoa wito kwa viongozi kujiepusha na siasa za ukabila na kuunga mkono umoja na maendeleo kwa minajili ya ustawi wa taifa hili.