Sekta ya utalii yachukua fursa ya maonyesho ya kitalii mjini Berlin

 

Sekta ya utalii hapa nchini inachukua fursa ya maonyesho ya kitalii mjiniA�A�Berlin, Ujerumani ili kuimarisha idadi ya watalii wanaozuru hapa nchini. Maonyesho hayo yatawezesha kampuni 42 za uchukuzi wa watalii hapa nchini kuonyesha vivutio vya watalii vya Kenya na kutoa fursa ya kushirikiana na kampuni kubwa za uchukuzi wa watalii na kupata ripoti za hivi punde za ujasusi kuhusu hali ya utalii duniani. Bara ulaya ndiyo chanzo kikuu cha watalii wanaozuru hapa nchini ambapo ilichangia asilima 36 ya jumla ya watalii waliozuru hapa nchini mwaka 2017. Wakati huo huo serikali inalenga kupitisha sheria muhimu zitakazoimarisha ustawi waA�A�sekta ya kifedha . Hazina kuu imebainisha mswada wa mpango utoaji mikopo , mswad wa halmashauri ya kifedha, msoko ya hisa , na mswada wa uwekezaji kuwa muhimu na ni miongoni mwa miswada inayotarajiwa kuimarisha sekta hiyo katika mwaka wa kifedha wa 2018/2019 . Hatimaye, waajiri wametakiwa kutumia teknolojia ya habari katika kutimiza mahitaji ya wafanyikazi wa kisasa. Shirikisho la waajiri nchini FKE linasema masharti mapya ya ajira yanapaswa kubuniwa kuambatana na wafanyikazi wa kiasasaA�A�ili kuboresha uzalishaji.A�Aidha; shirika hilo linaitaka serikali kubuni mazingira mwafaka kwa wale wanaio-anzisha biashara.