SebastiA?n PiA�era ashinda marudio ya uchaguzi wa Urais Chile

Tajiri mmoja wa kihafidhina na Rais wa zamani, SebastiA?n PiA�era, ameshinda marudio ya uchaguzi wa Urais nchini Chile. Mwana-saisa wa mrengo wa kushoto Alejandro Guillier alikubali kushindwa na kumpongeza mpinzani wakekufuatia ushindi huo na pia kurejea kwake katika wadhifa wa Urais baada ya kusalia nnje kwa miaka mine. Baada ya kuhesabiwa kwa karibu kura zote, PiA�era alikuwa akiongoza kwa asilimia 54. Ni uchaguzi ulioashiria mwanzo wa kuegemea upande wa kulia kwa taifa hilo ambalo kwa sasa linaongozwa na Rais wa Ki-socialisti Michelle Bachelet. Karibu watu milioni-14 walikuwa wamejiandikisha kupiga kura wakiwemo raia wa Chile wanaoishi ugenini kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo. Hata hivyo, idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa asilimia 48.5 pekee. Ilikuwa imebashiriwa kwamba kujitokeza kwa wingi kwa wapiga kura kungemnufaisha Guillier. PiA�era alitoa wito kuwe na umoja baada ya ushindi wake