Sasini limited kutafuta masoko mapya ya kahawa

Kampuni ya utayarishaji kahawa ya Sasini Limited imesema kuwa imezindua kampeini maksusi ya kutafuta masoko mapya ya zao hilo.Kampuni hiyo pia inataka kuimarisha masoko yake ya kawaida katika juhudi za kuboresha mapato ya wakulima.Mwenyekiti wa kampuni hiyo. Naushad Merali amesema kuwa anatumai kampuni hiyo itaweza kutumia fursa ya kuuza moja kwa moja asili 50 ya kahawa yake ugaibuni na kuimarisha mapato yake.Katika juhudi za kuzuia wakulima kupata hasara,kampuni hiyo ya sasini inapania kuimarisha mapato yake kwa kujihusisha na sekta nyingine kama vile ile ya maziwa.Hayo yanajiri huku wakulima wadogo wa kahawa huko Gititu katika kaunti ya Kiambu wakipata shilingi 1,033 kwa kilo moja ya kahawa ya hali ya juu.Soko la kahawa hapa Nairobi lilisema mwezi jana kuwa bei ya zao hili itapanda kutokana na kahawa ya hali ya juu inayokuzwa katika eneo la mlima Kenya.