Sarakasi yazuka baada ya viongozi wa NASA kujitokeza kuandikisha taarifa

Kulikuwa na sarakasi jana katika makao makuu ya idara ya upelelezi baada ya viongozi 12 wa muungano wa upinzani wa NASA kujitokeza kwa hiari kuandikisha taarifa kuhusu mashtaka mbali mbali yanayowakabili kama ilivyoagiza mahakama kuu. Hata hivyo maafisa wa makao makuu ya idara ya upelelezi katika jumba la Mazingira badala yake walikataa kuandikisha taarifa zao kulingana na agizo hilo la mahakama, wakisema viongozi hao sio wahusika kwenye jambo lolote. Hatua hiyo ilisababisha wabunge hao kuwalaumu maafisa hao wa upelelezi kwa kupuuza utawala wa sheria.

Wakili wao John Khaminwa alilalamika kwamba viongozi hao hawakufaulu hata kwenye jaribio lao na kuwasiliana na mkurugenzi wa idara ya upelelezi George Kinoti kwani hakuwepo ofisini. Miongoni mwa viongozi waliofika katika makao makuu ya idara ya upelelezi ni seneta wa Siaya, James Orengo, na mfanyibiashara, Jimmy Wanjigi, ambao serikali imetwaa hati zao za usafiri za paspoti na pia mbunge wa Dagoretti-kaskazini, Simba Arati na mwenzake wa Embakasi-mashariki

Kwa upande wake, Wanjigi pia aligusia lile suala la madai ya kutangzwa kifo chake na gazeti moja la humu nchini, akitishia kuwasilisha suala hilo mahakamani.