Santi Cazorla hatacheza msimu huu kwasababu ya jeraha la mguu

Kiungo wa Arsenal Santi Cazorla hatacheza tena msimu huu kwasababu ya jeraha la mguu. Cazorla hajacheza tangu alipoondoka uwanjani wakati wa mchuano wa makundi wa ligi ya vilabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Ludogorets uwanjani Emirates mwezi October. Aidha mchezaji huyo alifanyiwa upasuaji mwezi December huku kocha Arsen Wenger akitumainia kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 atarejea kabla msimu huu haujamalizika. Lakini mzaliwa huyo wa Uhispania sasa anaangazia kurejelea hali yake msimu ujao.