Sang Ndong Ateuliwa Kocha Wa Timu Ya Soka Ya Gambia

Aliyekuwa mchezaji wa kimataifa Sang Ndong ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Gambia kwa mara nyingine.Sang ambaye alijiuzulu katika timu ya Hawks inayoshiriki ligini nchini humo ameandikisha kandarasi ya miaka miwili na timu hiyo. Kocha huyo anachukua nafasi iliyoachwa na Raoul Savoy wa Uswizi aliyeondokaA� mwezi Disemba alipokubaliana na timu hiyo kukatiza kandarasi yake. Jukumu la kwanza la Ndong ni kuiandaa timu hiyo kushiriki katika mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika mwaka 2017 dhidi ya Mauritania mwezi ujao nyumbani na ugenini.Aidha kocha huyo alikuwa mkuu wa ushauri katika shirikisho la soka la Gambia na ameteuliwa mara kadhaa kuifunza timu hiyo siku za awali.A� Gambia kwa sasa inashikilia nafasi ya tatu katika kundi lao la kufuzu kwa fainali za kombe la bara Afrika ikiwa na alama moja baada ya kutoka sare baada ya kutofungana na Afrika Kusini, kisha ikashindwa na Kameruni bao moja kwa bila