Sakata Ya Nys Yaendelea Kumuandama Waiguru

Mshukiwa mmoja amedai kuwa aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru alihusika katika kashfa  ya shilingi milioni 791.Josephine Kabura Irungu amedai kuwa Waiguru alifahamu kuhusu  shughuli nzima ya malipo yaliofanywa kuhusu kazi iliofanywa na kwamba  pia alihusika  katika kuficha kashfa hiyo wakati uchunguzi kuhusu kashfa hiyo ulipoanzishwa.Madai hayo yanajiri siku chache baada ya Waiguru kuondolewa lawama kuhusiana na  kashfa hiyo na tume ya maadili na kupambana na ufisadi-EACC.