Safari Za Ndege Za Kati Ya Miji Ya Nairobi na Washington Huenda Zikaidhinishwa

KQ-DELTA-610x251
Serikali ya Marekani huenda ikaidhinisha safari za ndege za moja kwa moja kati ya miji ya Nairobi na Washington baadaye mwezi huu wakati waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani atakapozuru Kenya.
Waziri wa uchukuzi, James Macharia alisema Kenya imetimiza masharti yote yaliyowekwa na serikali ya Marekani.A�
Kenya inapania kutumia hatua ya kuidhinishwa kwa safari hizo za ndege kuboresha uhusiano wa kibiashara na utalii kati ya mataifa hayo mawili.A�