Safari ya Raila Uingereza yazua hofu

Mbunge wa Kuria Magharibi Mathias Robi ameelezea hofu kuhusu nia ya kinara wa muungano wa NASA Raila Odinga ya kuondoka humu nchini siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya wa urais. Robi alisema wakenya wameshikwa na hali ya mkanganyiko kwa sababu hawajui nia ya kiongozi huyo wa NASA kufuatia kuondoka kwake humu nchini wakati huu anapohitajika nchini. Mbunge huyo alidai kwamba lengo la upinzani ni kuzua wasiwasi na mkanganyiko humu nchini. Alisema chama cha Jubilee kimefanya kampeni zilizofaulu kote nchini huku wakiwa na imani kwamba watapata kura zaidi kuliko wakati wa uchaguzi wa urais wa Agosti 8. Robi aliunga mkono marekebisho ya sheria za uchaguzi zinazoshinikizwa na chama cha Jubilee akisema zinanuiwa kujaza pengo ambalo halikufafanuliwa kwenye katiba. Alidai kwamba ikiwa sheria zilizorekebishwa zitapitishwa na kutiwa saini na rais zitaruhusu kuapishwa kwa Rais mara tu anapotangazwa kuwa mshindi.

A�