Saad al-Hariri aibadili barua ya kujiuzulu kama Waziri mkuu

Waziri mkuu wa Lebanon Saad al-Hariri amesema leo kwamba ataahirisha kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu kufwatia ombi la rais Michel Aoun ili kuwezesha kufanywa kwa mashauriano zaidi .Hariri, ambaye alitangaza kujiuzulu kwake akiwa nchini Saudi Arabia,alionekana kando kando ya kaburi la marehemu babake,aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo aliyeuawa Rafik al-Hariri,mjini Beirut. Mapema alihudhuria sherehe ya maadhimisho ya uhuru baada ya kurejea nyumbani kwa mara ya kwanza tangu alipojiuzulu akiwa ziarani nchini Saudi Arabia.