Ruto awarai wafuasi wa Jubilee kujitokeza kwa wingi kumchagua rais Kenyatta

Naibu Rais William Ruto, amewarai wafuasi wa chama cha Jubilee kujitokeza kwa wingi na kumchagua Rais Uhuru Kenyatta wakati wa uchaguzi ujao wa Urais ambao utaandaliwa katika muda wa siku 60. Akihutubia wafuasi wa chama hicho mjini Thika, Ruto alisema kwamba chama cha Jubilee kiko tayari kuhifadhi ushindi wake. Ruto kwa mara nyingine alihimiza WaKenya kudumisha amani. Naibu Rais, alikuwa akihutubia wafuasiA� wa chama cha Jubillee baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili kwenye kanisa la Angiliokana la Saint Andrewa��s, mjini Thika.