Ruto awahimiza polisi kuyalinda maisha na mali ya wakenya

Naibu wa Rais William Ruto amewataka polisi kuyalinda maisha na mali ya wakenya wote. Naibu wa Rais aliwataka polisi kuharakisha katika uchunguzi na kuwakamata waliohusika na mauajiA� na uharibifu wa mali ili wachukuliwe hatua za kisheria. Akiongea katika kanisa la St Marka��s ACK, Mukui Parish katika eneo bunge la Kabete wakati wa sherehe za kuadhimisha mwaka wa 43 tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo, Ruto alizihimiza jamii mbali mbali kuishi kwa amani jinsi zimekuwa zikiishi bila kujali misimamo yao ya kisiasa. Naibu wa Rais aliwashauri wakenya kuwakataa wale wanaoeneza siasa za chuki, uchochezi, ukabila na migawanyiko miongoni mwa wakenya. Ruto alisema serikali itachukua hatua madhubuti ili kuhakikisha maisha na mali ya wakenya zimelindwa. Naibu wa Rais alisema hapana yeyote aliye juu ya sheriaA� na hatua zitachukulwa dhidi ya wale wanaowachochea wakenya kufanya ghasia bila kujali hadhi yao katika jamii,vyama vyao vya kisiasa au kule wanakotoka. Ruto aliwahimiza wakristo kuombea amani na uthabiti hapa nchini.