Ruto avunja kimya kuhusu uhusiano wake na Rais

Naibu wa raisA�A�William Ruto amevunja kimya chake na kuwaonya viongozi wa chama chaA�A�Jubilee kujiepusha na kile alichokitaja kuwa mijadala isiyokuwa na maana kuhusu uteuzi wa serikali na siasa za urithi za mwaka 2022. Ruto alisema kuwa viongozi wanapaswa kuangazia kutekeleza manifesto ambayo chamaA�A�hicho kilinadi kwa wakenya. Matamshi hayo yanafuatia mjadala mkali kuhusu sababu zilizomfanya kukosa kuhudhuria kikao cha wanahabari cha siku ya ijumaa katika ikulu ambapo rais Uhuru Kenyatta alitangaza sehemu ya baraza lake la mawaziri.